Jumapili 7 Septemba 2025 - 07:44
Kuuwawa kishahidi Waziri Mkuu na viongozi mashuhuri wa Yemen hakukuathiri mwendelezo wa mapambano ya Yemen

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanji alisema: Kuuwawa kishahidi Waziri Mkuu wa Yemen pamoja na viongozi wengine 21 mashuhuri wa Yemen hakukuathiri mwendelezo wa mapambano ya Yemen, bali mara moja serikali mpya iliundwa.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanji, Imam wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za Swala ya Ijumaa alizoitoa katika Husayniyya A‘zam Fatimiyya mjini Najaf Ashraf, alisema: “Kulikomboa bonde la Hauran baada ya miaka 21 – ambalo baada ya kuondoka majeshi ya Marekani na kuingia majeshi ya Iraq kwa msaada wa Hashd al-Sha‘abi, ambalo lilikuwa makao ya makundi hatari ya Daesh – ni ishara ya nguvu ya vikosi vyetu vya usalama na umuhimu wa Hashd al-Sha‘abi wetu.”

Imam wa Ijumaa wa Najaf Ashraf katika sehemu nyingine ya khutba alisema: “Shirika la Usalama wa Taifa hivi karibuni limechukua uamuzi bora wa kuwafuatilia kisheria wale wanaochapisha maudhui yasiyofaa. Huu ni uamuzi mzuri sana, na wakati wanataka kuchunguza maudhui yasiyofaa, tunawaomba pia watiwe moyo wale wanaochapisha maudhui yenye lengo na manufaa.”

Aidha, aliwashukuru wadau wote wa vyombo vya habari nchini Iraq na kuwaita askari wa mstari wa mbele katika vita vya kisaikolojia, akasisitiza kuwa kazi yao ni aina ya ibada katika kuitetea dini na taifa.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanji katika sehemu nyingine ya khutba alisema: “Kuuwawa kishahidi kwa Waziri Mkuu wa Yemen pamoja na viongozi wengine 21 mashuhuri wa Yemen hakukuathiri mwendelezo wa mapambano ya Yemen, bali mara moja serikali mpya iliundwa, hapa, tunapolaani kitendo cha kigaidi na cha woga cha Israel, tunawapongeza na kuwapa pole watu wa Yemen kwa mashujaa wao hawa, pia tunatoa heshima na shukrani zetu kwa Sayyid Abdul Malik al-Houthi – Mwenyezi Mungu amhifadhi – kwa msimamo wake wa kishujaa na wa ajabu.”

Kuhusu majanga yaliyotokea Afghanistan na Sudan alisema: “Wiki iliyopita tetemeko la ardhi lilitokea Afghanistan na kusababisha vifo vya watu 1,400 na uharibifu wa nyumba 5,000. Pia, maporomoko ya ardhi yalitokea Sudan na kusababisha vifo vya watu 1,000.”

Aliongeza kuwa: “Tunawasilisha rambirambi zetu kwa watu wa Afghanistan na Sudan kwa misiba hii miwili.”

Imam wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, kuhusu masuala ya kimataifa, alisema: “Trump, Rais wa Marekani, amebadilisha jina la Wizara yake ya Ulinzi na kuipa jina la Wizara ya Vita, jambo linaloashiria tangazo la vita, mabadiliko haya yana athari nyingi, lakini tunamwambia: Mali zenu hamtozifaidi, na chochote mtakachofanya, sisi tutakabiliana na vita vyenu, hatutaanzisha, lakini tuko tayari kujibu.”

Khatibu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf katika khutba ya kidini alikumbusha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (saw) na akasema: “Yeye ndiye mwisho wa Mitume wa Mwenyezi Mungu, kwani baada ya Uislamu hakuna dini nyingine, na leo tupo katika alfajiri ya karne ya kumi na tano baada ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (saw).”

Aliendelea kusema: “Mustakabali wa wanadamu wote uko mikononi mwa Imamu wa Kumi na Mbili (aj), ambaye ni mmoja wa kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).”

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanji katika sehemu nyingine ya khutba alisema: “Tumemaliza ziara ya Imamu Hasan al-‘Askari (a.s.), ambapo vyanzo rasmi vimehakikisha kuwa mazuwari milioni nne – wote wakiwa ni Wairaqi – walihudhuria, hapa, tunashukuru mashirika ya kiraia, ya afya na huduma, familia na mawakibu kwa kufanikisha ziara hii ya mamilioni.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha